Msake Mpaka Umpate

by Augustine L. Sangi


"Ningependa ufanye upelelezi wa uhalifu huu. Msake mhalifu mpaka umpate. Ninakuamini kwamba unaweza kumnasa mhalifu huyo kutokana na uhodari wako katika kazi hii. "Kwa bahati nzuri, mtu mmoja alinusurika kati ya hao waliokumbwa na mkasa huu. Risasi za jambazi zilimkosa na akajifanya amekufa." Tom... Alitega sikio na kumsikiliza mkuu wake wa kazi akiendelea: "Huyu bwana aliyenusurika ndiye aliyetoa taarifa ya ujambazi huo kituoni, na jina na anwani yake ni hivi..." Tom alioneshwa kikaratasi kilichokuwa na maandishi ya mkono yenye taarifa hii: Jina - Deo Pantaleo, Mtaa -Swahili, Namba ya nyumba - 85, Shauri - KJ/II/66. 

ISBN: 9789966310675 SKU: 2010143000836
KES 530
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect

Reviews

This product does not have any reviews yet.

Add your review