Phoenix Hatua za Kiswahili Rasmi GD3 (Approved)

by "Momanyi, Mutuku"


Hatua za Kiswahili Rasmi, Kitabu cha mwanafunzi ni mfululizo wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa ufundi kwa kufuata mtalaa mpya unaosisitiza umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunz: kukuza weledi wake katika stadi za kusikiliza na kuzungumza, sarufi na matumizi ya lughakusoma na kuandika. Vitabu hivi vina sifa zifuatazo:

 

- Mada kuu zilizopangwa kwa kuzingatia ruwaza ya mtalaa ya Kiswahili Gredi ya 3 ili kurahisisha utumiaji.

- Vipindi vilivyopangwa kushughulikia mada ndogo mbalimbali kulingana na ruwaza ya mtalaa.

- Picha na michoro iliyochorwa kwa rangi za kupendeza ili kuvutia usomaji na ujifunzaji.

-  Maswali dodoso yanayochochea uwezo wa mwanafunzi kufikiria na kudadisi masuala mbalimbali.

- Kazi za ziada na majaribio yanayomhusisha mwanafunzi binafsi, wanafunzi wawiliwawili na wanafunzi kwenye makundi katika shughuli ainaaina.

-  Mradi wa nyumbani unaowahusisha wazazi na walezi katika ujifunzaji wa Kiswahili na pia kukuza uwajibikaji.

-  Hadithina utajiri wa shughuli nyingine zinazokuza umilisi wa kimsingi wa lugha ya Kiswahili na zilizooanishwa na masuala mtambuko, maadili chanya miongoni mwa masuala mengine.

- Matumizi ya teknolojia kwa mfano kusikiliza sauti redioni na unasaji sauti kwa kutumia simu na vifaa vingine vya kiteknolojia.

ISBN: 9789966479327 SKU: 2010127000755
KES 638
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect