OUP Kiswahili Dadisi Mazoezi Gredi 3 (Toleo Jipya)

by Oxford


Kiswahili Dadisi ni msururu wa vitabu vilivyoandikwa kwa utaalamu na upekee ili kufanikisha ufundishaji na ujifunzaji wa mahitaji ya Mtaala wa Umiblisi. Vitabu hivi vitawawezesha wanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika, na vilevile Sarufi, kupitia mazoezi murua ambayo pia yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala mtambuko.

Katika Kiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 3, utapata:

-mada zilizopangwa kwa kuzingatia muainisho wa mtaala.

-mifano halisi ya matumizi ya lugha kimuktadha.

-mazoezi ya kuchangamsha na_ kufikirisha ambayo yanawashirikisha wanafunzi moja kwa moja.

-vifungu vya kuburudisha na vinavyoendeleza ujifunzaji.

-nyimbo za kusisimua ambazo zitawachangamsha na kuwaburudisha wanafunzi.

-picha za rangi, zenye mvuto wa kipekee na ambazo zinachangia pakubwa katika ujifunzaji wa mwanafunzi.

-mazoezi ya kuwahamasisha wanafunzi kuendeleza ujifunzaji nje ya darasa.

-Mazoezi ambayo yatawashirikisha mwanafunzi kutumia vifaa vya kidijitali katika ujifunzaji.

-jinsi ya kumshirikisha mzazi au mlezi kuimarisha ujifunzaji.

ISBN: 9789914441420 SKU: BK00000011295
KES 551
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect