Storymoja: Hatua ya Jesa

by Erick Livumbazi Ngoda


Wazazi wa Jesa wanapotengana, Jesa anaishi na mama yake ambaye baadaye anapata ajali ya barabarani. Jesa, msichana mwenye umri wa miaka kumi na sita, anaishia kuwa tegemeo la familia yake kiuchumi. Hana _ budi kutafuta riziki kwa kufanya kazi ya ujakazi ili kumtunza mama yake. Licha ya hayo, ana kipaji na ari ya kucheza kandanda. Je, atafaulu kupata timu ya kuichezea huku akifanya kazi?

Hatua ya Jesa ni novela inayoangazia changamoto anuwai zinazowakabili vijana katika jamii kama vile athari za migogoro ya kifamilia, ajira kwa watoto, matatizo ya kiuchumi na ukosefu wa mikakati kabambe ya kukuza vipaji wa vijana katika jamii.

ISBN: 9789966623614 SKU: BK00000005553
KES 480
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect