Longhorn Kiswahili Mufti Kitabu Cha Mwanafunzi Gredi 3

by Longhorn Publishers


Longhorn Kiswahili Mufti, Gredi 3 (Kitabu cha Mwanafunzi) ni kitabu kilichoandikwa kwa mtindo wa mazoezi kwa kuzingatia mtaala mpya unaokusudiwa kujenga ujuzi wa mwanafunzi kupitia utendaji na uvumbuzi wa maarifa. Kitabu hiki kimetimiza kikamilifu mahitaji ya mada zote za silabasi mpya ya somo la Kiswahili kwa wanafunzi wa gredi ya tatu.
Vilevile, kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha rahisi ili kueleweka kwa urahisi na wanafunzi wa gredi ya tatu kutoka katika mazingira mbalimbali. Msamiati uliotumika unaafikiana vyema na uwezo wa lugha ya wanafunzi katika kiwango hiki. Kimeshughulikia masuala ibuka kama vile: maadili, haki za watoto, afya bora, uraia, ujasiriamali, elimu endelevu, teknolojia na mazingira.
Kadhalika, michoro ya kuvutia imetumiwa ili kumsaidia mwanafunzi kufahamu yaliyomo kwa urahisi na kuweza kuyahusisha maarifa na mazingira.

ISBN: 39789966640048 SKU: 2010127000742
KES 516
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect