JKF Nyota ya Kiswahili Grade 3 (Approved)

by "Salim, Nganje"


Kitabu hiki kimedhamiriwa kutumika kama mfululizo wa vitabu vya kiada kwa Gredi ya Tatu. 
Kimeandikwa kuambatana na mtalaa mpya. Kitabu hiki kimelenga kumwongoza mwanafunzi katika masomo yake ya lugha ya 
Kiswahili kwa kutimiza maarubu ya mtalaa wa kiwango husika. 
Ndani yake mna mbinu bora za ujifunzaji ambazo zitawaelekeza wanafunzi kuhusu njia bora za kutimiza malengo yao. 
Kimezingatia stadi zote za kujifunza lugha, yaani: 
(i) Kusikiliza 
(ii) Kuzungumza
(iv)Kusoma
(vi)Kuandika
(v)Msamiati
(vi)Sarufi
Mwanafunzi amepewa nafasi ya kujifunza mwenyewe kutokana na picha maridhawa, 
hadithi, mashairi na michezo murua. Ili kuzidisha hamasisho la ujifunzaji, 
mwongozo maalumu umeandaliwa ili kuwapa walimu mbinu thabiti za kuuchochea ujifunzaji miongoni mwa wanafunzi. 
Ili kutathmini kiwango cha ujifunzaji miongoni mwa wanafunzi kitabu hiki kimetoa mazoezi ya kutosha 
yatakayowawezesha kupata: 
- Umilisi wa kimsingi
- Maadili ya kimsingi
- Uwezo wa kuyashughulikia masuala mtambuko

ISBN: 9789966511478 SKU: 2010127000794
KES 452
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect