Lulu Za Fasihi: Njozi Yapata Mtenzi

by Mwenda Mbatia


Njozi Yapata Mtenzi ni riwaya ambayo ina simulizi yenye mikondo kadha inayoingiliana. Mkondo mkuu unamhusu Kiguto. Kiguto ni kijana hodari masomoni, jamali wa sura na mwana wa jadi kubeli.

Ana vipawa na nafasi nyingi za kujiendeleza maishani, ikiwa ni pamoja na kujiunga na chuo kikuu cha nchini au cha ng’ambo.
Anapojiunga na mafunzo ya polisi kazi inayodharauliwa, anawashangaza wengi. Sababu yake ya kufanya hivyo ni kufuata
ndoto yake. Je, atatimiza ndoto hiyo au ataambulia patupu?

Hii ni riwaya inayotumia mbinu na mikakati anuwai kumzindua msomaji kuhusu changamoto na manufaa ya uhuru wa kimawazo. Inawafunza vijana kwamba wanaweza kuibadilisha mitazamo hasi ya wanajamii kuhusiana na baadhi ya taaluma na ajira. Kuweza kufanya hivyo, kunahitaji ndoto kuu na ujasiri mkubwa wa kuzifanikisha. Mitindo ya riwaya ya upelelezi, ya kijasira na ya kijamii imetumiwa sawia kuwasilisha yaliyomo.

ISBN: 9789966631701 SKU: 2010143001005
KES 400 KES 632
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 3,000
Free click & collect

Reviews

This product does not have any reviews yet.

Add your review