Msimamo Kamili!:Habari na visa kuhusu Ukimwi

by Francis Taylor


Mtu yeyote anaweza kupatwa na UKIMWI. Wewe unaweza kupatwa na UKIMWI. Ili kuzuia ugonjwa wa UKIMWI usienee, ni lazima tuzungumze na tuzieleze habari za ugonjwa huu. Hii ndiyo sababu inayotufanya tuongee habari za UKIMWI sasa.Pia, tunahitaji kuongea juu ya yale mambo yote mabaya ambayo watu wanayafanya. Mambo haya mabaya yanasambaza virusi vya HIV kwa watu wengi sana. Tutaweza kuzuia kuenea kwa UKIMWI kama tukiacha kuyafanya hayo mambo mabaya ambayo hueneza virusi. Vile vile tunahitaji kuongea juu ya njia zinazofaa za kuwatunza watu wetu wanaougua UKIMWI.Watu wengine wamechanganyikiwa. Watu hao huongea mambo ya kijinga kuhusu kuonana kimwili kwa mume na mke. Usiwaruhusu watu hao wakubabaishe akili. Fanya ujasiri wakuwaondokea. Waache. Visa na majadiliano yaliyomo ndani ya hiki kitabu yatakuongoza kujua jinsi ya kuwaepuka watu hao. Kwenye hadithi unazosimuliwa humu ndani, pengine unaweza kuona kisa kimojawapo ambacho kimekupata wewe mwenyewe au kimempata rafiki yako.

ISBN: 996688257X SKU: 2010143000528
KES 174
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 3,000
Free click & collect

Reviews

This product does not have any reviews yet.

Add your review