Isimujamii (focus)


Isimujamii ni kitabu kinachoangazia maswala ya mahusiano yaliyopo baina ya lugha na jamii na vilevile jinsi jamii inavyotumia lugha. Mada za kitabu hiki zinahusu maelezo ya taaluma ya isimujamii, umuhimu wake na jinsi ambavyo masiala mbalimbali yanavyopelekea matumizi ya lugha kujipambanua. Kitabu chenyewe kinafafanua maswala mengi yanayohusu lugha na jamii. Juu ya hayo, kitabu hiki pia kinaangazia dhana muhimu zitumiwazo katika taaluma ya isimujamii kama vile lugha, lahaja, lafudhi, sajili na msimbo. Jambo lingine muhimu ambalo limefafanuliwa ujuzi wa lugha katika jamii ambapo mambo kama umojalugha, uwililugha, wingilugha, daiglosia nk yanajitokeza. Katika Isimujamii pia kuna maelezo juu ya majukumu ya lugha katika jamii, upangaji lugha na sera ya lugha. Haya ni mambo ambayo kwa muda mrefu hayakutiliwa umuhimu yanayostahiki hususani katika asasi zetu za elimu. Hill ni pengo kubwa hasa ikichukuliwa kuwa lugha ni mali ya jamii na kwamba kuna uwezekano wa kutokuwepo lugha kama jamii haipo. Kitabu hiki kinakusudiwa kusaidia kujaza pengo hili. Kwa sababu hiyo, Isimujamii ni nguzo muhimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu (katika viwango vya shahada ya kwanza na uzamili). wa vyuo vya uatimu na pia wale wa shule za upili. Kitabu hiki pia kitawafaa walimu wa Kiswahili pamoja na wote wanaokienzi Kiswahili. 

 

 

KES 464
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect