KLB Early Grade Kiswahili Mazoezi ya Lugha Gredi 3


Kitabu hiki cha Kiswahili Mazoezi ya Lugha cha Gredi 3 hutumia mbinu za ujifunzaji ambazo zimefanyiwa utafiti. Mbinu hizi zitamsaidia mwanafunzi kukuza stadi za lugha ambazo hatimaye husaidia ukuzaji wa umilisi wa kimsingi, ukuzaji wa maadili na utekelezaji wa shughuli za kijamii pamoja na kuzingatia masuala mtambuko. Masuala makuu yaliyo katika kitabu hiki yametumiwa kama chombo cha kukuza stadi nne za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika.

Uandishi wa kitabu hiki umezingatia uhusishi wa vipengele vyote vya Mtaala wa Kiumilisi ambavyo huchangia ujifunzaji katika lugha ya Kiswahili. Mwanafunzi wa Gredi ya 3 amepewa nafasi ya kujifunza kutokana na tajriba mbalimbali na tathmini ambazo humwezesha kudhihirisha umilisi wa kimsingi na kuwa na maadili yanayotarajiwa katika lugha ya Kiswahili.

Kitabu hiki kimeegemea na 444 kuzingatia tajriba zinazotokana na mradi wa Wizara ya Elimu wa Tusome. Mradi huu umefadhiliwa na shirika la USAID. Inatarajiwa ya kwamba mwanafunzi atakayekamilisha yaliyomo kwenye kitabu hiki atakuwa na uwezo wa kusikiliza na kuzungumza ipasavyo, kusoma kwa ufasaha na kwa mtiririko ufaao, na hata kuandika.

ISBN: 9789966656322 SKU: BK00000005948
KES 406
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 3,000
Free click & collect