Rozi anajuta

by Story Moja

by Pauline K Kyovi


Hadithi hii inawafundisha watoto wanaokosa kuomba msamaha. Tena inawafundisha watoto kuwa makini wanapotumwa kwenye duka. 
Msomaji pia atakuza msamiati na ufahamu wake.
SOMA PAMOJA NA MTOTO WAKO
Furahia uhondo wa kusoma pamoja na mtoto wako. 
Mtoto wako atavipenda vitabu maishani mwake na atajifundisha kwa wepesi endapo 
utazingatia hoja kumi rahisi zilizoorodheshwa hapa chini. 
1. Soma pamoja na mtoto wako katika mazingira yaliyotulia kama vile
kwenye chumba cha kulala. 
2. Mhimize mtoto wako awe na mazoea ya kusoma hadithi nzima kwa kutumia
viziada vya lugha kama vile kupandisha sauti. Asome hadithi nzima
kwanza akilenga kuifurahia tu kisha aisome tena ili ajue yaliyomo. 
3. Mhimize mtoto wako ayaashirie maneno kwa vidole hasa anaposoma hadithi
aliyokwisha kuisoma awali. 
4. Chunguza kama mtoto wako anaelewa aliyoyasoma kwa kumuuliza maswali
rahisi kuhusu michoro, wahusika na hadithi kwa jumla. 
5. Kuwa na mtazamo chanya kuhusu hatua anayopiga mtoto wako katika usomaji
wake. Usimvunje moyo bali umsifu kwa kila hatua anayopiga. 
6. Hakikisha kwamba mtoto wako anaisoma hadithi mara kadhaa. 
7. Baada ya mtoto wako kuzoea kusoma hadithi fulani, mhimize ajaribu kukusomea
baadhi ya maneno ya hadithi hiyo au hadithi nzima. 
8. Mnunulie mtoto wako vitabu tofauti tofauti vya kuburudisha kama vile
vitabu vya picha, vya kuchekesha na vya kuelimisha. 
9. Mwonyeshe mtoto wako kwamba una nia ya kufuatilia na kujua hadithi
anazozisoma kwa kumuuliza maswali kuhusu hadithi hizo. Pia mhadithie
hadithi ulizosoma kwenye vitabu ulivyo navyo. 
10. Uwe kielelezo bora kwa mtoto wako ili avithamini vitabu. Mwache mtoto
wako akuone wewe ukisoma vitabu vingi.


 

ISBN: 9789966066763 SKU: 2010143001028
KES 420
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect