Wimbo Mpya

by Mwenda Mbatiah


Wimbo Mpya ni riwaya inayomulika kipindi mahsusi na cha kipeo katika historia ya Kenya. Mwandishi anakitupia jicho la tahakiki kipindi cha mpito baina ya harakati za kuung'oa ukoloni na uhuru. Anazua maswali ambayo yamekataa kusahaulika. Je, majilio ya uhuru yalileta ushindi au ushinde kwa wapiganaji walioendesha vita vya msituni dhidi ya jeshi na masetla wa Kiingereza? Je, serikali mpya ya Mwafrika ilitimiza au iliva ndoto ya wananchi? Je, wananchi wa kawaida vijijini waliupokeaje wito wa viongozi wa Kenya huru - wito wa kushirikiana katika moyo wa harambee kupigana vita na maadui wa ujinga, maradhi na umaskini? Wanawake hawaachwi nyuma katika tendo la kihistoria la Kenya kuvuka kutoka enzi ya harakati za ukombozi hadi enzi ya wimbo mpya wa uhuru na ujenzi wa taifa.

ISBN: 9966223789 SKU: 2010143000274
KES 344
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 3,000
Free click & collect