EAEP Akili Pevu Kiswahili Teacher's Grade 8


Akili Pevu Kiswahili Kitabu cha Mwalimu, Gredi ya 8 ni kitabu kilichotungwa kwa upeo wa ubunifu na kuwambwa kwa makini. Kimetimiza kwa ukomo wa ukamilifu mahitaji ya Mtaala wa Kiumilisi. Kitabu hiki kinafafanua yaliyomo katika Akili Pevu Kiswahili Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 8.

Mwalimu ni wenzo muhimu katika utekelezaji wa mtaala huu. Mwongozo huu hivyo basi unatoag mwelekeo ufaao kwa kumwongoza mwalimu hatua kwa hatwea katika ufundishaji. Mwongozo huu unajumuisha:

-Utangulizi unaofafanua kwa kina vipengele muhimu vya Mtaala wa Kiumilisi.

-Kielelezo cha maazimio ya kazi pamoja na andao la somo kwa kutumia mtindo mpya uliopendekezwa na KICD.

-Mapendekezo ya jinsi ya kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitgji ya kipekee darasani.

-Utangulizi kwa kila mada. Kabla ya vipindi vyenyewe, mwalimu anaonyeshwa matokeo maalum yanayotarajiwa katika kila mada, umilisi wa kimsingi unaokuzwa, uhusiano na masomo mengine, uhusiano na masuala mtambuko, maadili, nyenzo za kufundishia na mbinu za kutathmini wanafunzi pia zimeshirikishwa ndani ya shughuli.

-Majibu kamili ya mazoezi pamoja na maelekezo kwa mwalimu kuhusiana na shughuli teule.

-Viwango ambavyo mwalimu anazingatia anapowatathmini wanafunzi wake.

Mwongozo huu umeandikwa kwa utaalamu na waandishi wenye tajriba na uzoefu mwingi katika uandishi.

KES 986
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 3,000
Free click & collect