Hujafa Hujaumbika

by Kagwa


Mwanga, almaarufu ‘Fumo’, ni kijana mdogo ambaye hana hakika na asili wala fasili yake. Yeye ni msi baba, msi mama. Anachokifahamu ni kwamba ‘aliokotwa’ kutoka katika makao ya mayatima. Licha ya kuwa yeye ni kiokote, mtezi wake anampa kila kinachostahili kwa mtoto mwenye wazazi wote.

Hali inapoonekana kutakata, msiba baada ya msiba unabisha. Mlezi wake wa pekee ambaye anamjua kama ‘mama’ anapigwa kalamu. Nyumba yao inauzwa kwa wenye nacho. ‘Dada yake’ Fumo ananajisiwa na kubaki hali mahututi katika mshikemshike wa kufurushwa kutoka kwa nyumba yao na wahuni watioletwa na mmiliki mpya. Baadaye, mlezi wa Mwanga anafunguliwa mashtaka ya kusingiziwa ili asiweze kufuata kesi ya kufutwa au kufurushwa kutoka kwa nyumba yake. Mwanga na ‘familia’ yake wanajipata katika mitaa ya vitongoji duni. Choo ni cha "kurusha fataki" na bafu ni upenuni. Hamna stara tena!

Akiwa shuleni, Mwanga anafanya bidii ya mchwa na kupita vyema, lakini mikosi bado haimwachi akapumua. Huku akicheza na watoto wengine, anajipata amekanyaga kilipuzi na kupoteza mguu wake. Lakini bidii yake na  kudura za Mwenyezi Mungu vinamwezesha kuwa mwanasheria nguli. Azma yake sasa ni kutetea haki licha ya kilema chake. Kumbe kufa si kufariki, kufa ni kuoza utumbo!

Hii ni riwaya ya kusisimua yenye kutia matumaini katika jamii iliyotamauka kutokana na matatizo mengi yanayoletwa na ufisadi na kupotoka kwa maadili.

ISBN: 9789966315687 SKU: 2010143001043
KES 612
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect