Wasakatonge

by Oxford


Wasakatonge ni diwani yake mpya yenye hazina ya mashairi yenye kubainisha sauti kali ya utetezi kwa wavujajasho wanaonyanyaswa, kuonewa, kudharauliwa na kunyonywa nguvu zao. Ni kauli inayobainisha uoza wa jamii na athari zake kwa wanyonge. Diwani hii ni chachu ya kuuzindua umma ulioghilibiwa iii udai haki yao dhidi ya wanasiasa madikteta wanaotumia nguvu za dola kwa maslahi yao. 

Kitabu hiki mbali ya kuwa na kina kizito cha maudhui, fani yake pia imetia fora. Kwa wale wapendao ushairi "bulibuli" wa Kiswahili hiki ndicho kitabu chao. Wanafunzi wa sekondari, vyuo na vyuo vikuu watafaidika sana wasomapo diwani hii. 

Mwishoni mwa kitabu hiki, kuna orodha ndefu ya maneno na mama zake ambayo bila shaka yatakuwa hazina kubwa katika kuyafaidi na kuyaelewa ipasavyo mashairi haya. 

ISBN: 9789976400243 SKU: 2010129000099
KES 464
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect