Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza Tuki Toleo la pili
by Tuki
Hili ni Toleo la Pili la Kamusi ya Kiswahili Kiingereza. Toleo la Kwanza lilichapishwa mwaka 2001. Mara baada ya kuchapishwa kwa Toleo la Kwanza la kamusi hii, wataalamu wa Leksikografia wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walianza zoezi la kutafuta maoni ya watumiaji wa Toleo la Kwanza la kamusi hii. Maoni ya watumiaji mbalimbali wa Toleo hilo kutoka ndani na nje ya nchi yalipokelewa na kufanyiwa kazi. Aidha, kamusi hii imepitiwa na kuhakikiwa na wataalamu wa lugha na isimu kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania na Kenya. Udurusu wa Toleo la Pili ulianza mwaka 2004 na kukamilika mwaka 2014. Kamusi hii itawafaa sana wanafunzi na walimu wa sekondari na vyuo, watafiti, wataalamu na wazungumzaji wa lugha za Kiswahili na Kiingereza. Imesheheni methali za Kiswahili na visawe vya Kiingereza, vinyambuo vya vitenzi vimefafanuliwa na mifano mingi ya matumizi imetolewa.