Longhorn: Sudi Atekwa Nyara Grade 3

by Wekesa


Baada ya kufanya vizuri katika mtihani, Sudi na Shada wanapelekwa na wazazi wao kwenye mbuga ya wanyama. Wanapofika mbugani, Sudi anatoweka pasi na yeyote kumwona. Wazazi wake na dada yake wanaanza kumtafuta. Je, Sudi anapatikana?

Hadithi Mufti za Longhorn ni mfululizo mpya wa hadithi ambazo zimeandikwa kulingana na mtaala mpya. Hizi hadithi zinalenga kukuza ujuzi wa wanafunzi kupitia kwa uvumbuzi wa maarifa na zinaimarisha uelewa wao wa masuala ibuka katika jamii. Hadithi hizi sio tu za kuelimisha na kuburudisha, bali pia zimeambatanishwa na mazoezi ambayo yatawasaidia wanafunzi kuimarika kiubunifu, kimawazo na kifikra.

ISBN: 9789966642110 SKU: 2010143001091
KES 258
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect