Made Familiar: Mwanzo mpya na Hadithi nyingine Level 7

by Made Familiar


Omari, ambaye ni kijana anayeishi mtaani, amekuwa na mazoea ya kuwaibia watu katikati ya jiji. Mara hii, ameibia mtu asiyekuwa wa kawaida. Siku zake za arubaini zimefika. Umati wa watu uliojihami kwa kila aina ya silaha unamfuata unyounyo. Jambo linalomshangaza Omari na umati huu ni kwamba aliyeibiwa simu anataka Omari asiadhibiwe. Mtu huyu ni nani? Je, huu ni mwanzo wa mabadiliko katika maisha ya Omari au maisha yake yataangamia?

Kwingineko, Tim na Nim wamefunga safari ya kuzuru Nyasaland ili kutafutia mifugo yao maji na malisho. Huko, wanakutana na Naseko ambaye pia ana lengo lile Lile. Pale, wanapata tangi maalumu ya maji ambayo licha ya kutumia maji yake kwa muda mrefu, haishi maji. Kisha, ghafla, tangi inakauka. Ukame mkubwa unakumba Nyasaland. Watafanya nini?

Kitabu hiki kinakuza ufunzaji na ujifunzaji wa mada kama vile crop production, animal handling, water conservation na soil
pollution (Agriculture); Money (Business Studies). Pia, kitabu hiki kinakuza umilisi na maadili kama vile uwajibikaji, kujiamini, heshima, upendo, uwazaji kina na ubunifu jinsi ilivyopendekezwa katika mtaala mpya.

ISBN: 9789914997521 SKU: BK00000011216
KES 375
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect