Mwongozo wa Nguu za Jadi (Globalink)


Mwongozo Kamilina wa Kina wa riwaya ya Nguu za Jadi

Mwongozo huu wa kina na wa kipekee wa riwaya ya Nguu za Jadi ni tofauti sana na miongozo mingi ya hapo awali. Hii ni kwa sababu unashughulikia maswali kama vile ploti (msuko), mandhari pamoja na umuhimu wake ambayo hapo awali yalikuwa yanapuuzwa. Haya siku hizi yanatokea katika mitihani ya kitaifa ya ya Karatasi ya tatu ya Kiswahili (F asihi). Upekee mwingine ni kwamba, unafuata kanuni za mtindo mpya wa utahini katika karatasi hii ya tatu. Maswala mengine ambayo yameshughulikiwa na mwongozo huu ni ufaafu wa jalada na anwani wa riwaya hii, dhamira, maudhui, wahusika na mitindo mbalimbali ya matumizi ya lugha na uandishi (Tamathali za usemi na Sanaa). Vipengele hivi vyote vimetolewa maelezo pamoja na mifano kochokocho.

Aidha, mwishoni wa riwaya hii kuna mengi ya maswali ya mukhtadha, maudhui, wahusika na mtindo. Kando na maswali haya, kuna maswali mengine ya mwingiliano wa vipengele vya kifasihi kama vile ploti, mandhari, maudhui, wahusika na mbinu za kimtindo. Maswali haya yanapatikana katika utahini wa mitihani ya kisasa ya kitaifa. Maswali haya yote yameshughulikiwa kwa ukamilifu na kwa kina. Kwa hakika huu ni mwongozo wa kipekee kwa mwalimu na mwanafunzi anayetaka kunoa makali yake katika uwanja wa Fasihi.

ISBN: 9789966766939 SKU: BK00000008600
KES 522
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect