Narejea Nyumbani

by JKF


"Mtindo wa uandishi katika nafsi ya kwanza unatilia uzito uhalisia wa riwaya ya Narejea Nyumbani. Hii ni hadithi ya kuzua mjadala kuhusiana na maisha ya mwandishi, hasa kutokana na mbinu rejeshi iliyotawala kisa chote. Ni hadithi inayomsukuma msomaji kutoka kipembe hiki cha maisha hadi kile kingine." Prof. Ken Walibora, Chuo Kikuu Cha Wisconsin-Madison, Marekani, 21 Julai 2012. 

"Hii ni riwaya ya pekee inayosimuliwa katika nafsi ya kwanza. Ukabila unabainika kuwa chanzo cha mzozo katika ndoa. Ndoa si agano tena. Ni mchezo wa 'Naja Leo, Naenda Kesho:Tatizo hili litapata utatuzi mwafaka lini? Hi ni hadithi kuntu." Bi. Sheila Kiplagat, Kabartonjo,14 Agosti 2012. 

"Blla kuandika hadithi hii, basi Jeff Mandila angesalia kuwa bubu wa ujumbe ambao .huenda ungeudhuru moyo wake uliozoea kusema ukweli namna alivyozoea kusema marehemu baba yake." 8w. Lazarus Fundia, Busia, 2 Novemba 2012. "Ni nini kilichonifanya kuingia katika pendo ambalo halikuwa la dhati? Pendo haramu. Pendo la fisi mla watu? Ni nini? Najuta kumpenda asiyependeka." 

ISBN: 9789966510266 SKU: 2010143000806
KES 565
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect