Storymoja Smart Beginners Cheche za Kiswahili Gredi 3
Cheche za Kiswahili: Kitabu cha Mwanafunzi kwa Gredi ya 3 kimeandikwa kwa kuzingatia yaliyomo kwenye ruwaza ya Mtaala wa Kiumilisi (CBC) ili kumfaa mwanafunzi kutekeleza shughuli mbalimbali za ujifunzaji. Shughuli zilizopendekezwa katika kitabu hiki zitamwezesha mwanafunzi kuwa na umilisi wa stadi mbalimbali.
Sifa zake kuu:
-Vipengele vyote vya mada mbalimbali kwa mujibu wa ruwaza ya mtaala.
-Picha na michoro angavu kwa qjili ya kumwezesha mwanafunzi kuelewa matini.
-Shughuli tagusani kuhusu mada mbalimbali kwa mujibu wa ruwaza ya mtaala mpya.
-Uhusishaji wa shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji.
-Ujumuishaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli za ufunzaji na ujifunzaji wa Kiswahili.
-Ushirikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
-Ujumuishaji wa masuala mtambuko katika shughuli za ujifunzaji.
Waandishi wa kitabu hiki ni walimu wenye tajriba pana katika ufundishaji wa Kiswahili katika kiwango cha shule za msingi.
UPC | BK00000010949 |
---|---|
Author | Storymoja |
ISBN | 9789914466652 |
SKU | BK00000010949 |