Darubini ya Utunzi


Uandishi ni stadi inayohitajika popote tulipo maishani. Barua,memoranda, kumbukumbu na ripoti rasmi, miongoni mwa mengine, ni maandishi yanayohitajika kila siku katika mwahali
mwa kazi. Licha ya kumwelekeza mwanafunzi katika kila aina ya uandishi
unaohitajika katika kujitayarisha kwa KCSE, Darubini ya Utunzi pia kinamtayarisha kwa maisha ya baadaye. Kinapiga darubini mahitaji yote ya uandishi, tangu insha hadi uchambuzi wa fasihi, 
na kitazifaa sana shule za upili na vyuo vya walimu. Vilevile, ni utangulizi muhimu kwa wanafunzi wa Kiswahili
katika miaka ya awali ya chuo kikuu.
Dkt. John Habwe ni mhadhiri Mwandamizi wa Isimu na Lugha katika Chuo Kikuu cha Nairobi, ambako alijipatia shahada za B.A, M.A na Ph.D. 
Licha ya kuwa ameifunza lugha na fasihi ya Kiswahili katika ngazi tofauti, ni mwandishi mtajika wa
riwaya, hadithi fupi na vitabu juu ya ufundi wa lugha.
 

ISBN: 2010127000365 SKU: 2010127000365
KES 597
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect