Masomoni California


Mureti na Mugiira wanapopata ufadhili wa kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha California, Marekani wanafurahi sana.
Wanaabiri ndege kwa mara ya kwanza na wanaajabia mengi wanayoyaona katika safari yao hadi Marekani. Lakini maajabu ya 
kweli yanawasubiri California wanakokwenda kusoma. Mapokezi na mlahaka mwema wanaopata kutoka kwa Profesa Kithaka unatiwa 
doa na wasichana wawili wa Kimarekani; Mary Anne na Brigit wanaotaka mapenzi ya lazima kutoka kwa Mureti na Mugiira.
Mary Anne na Brigit wanafanya mipango ya kuwateka Mureti na Mugiira, kwa bastola au hata kwa mkataba (kama alivyotekwa 
kijana mmoja wa Kiafrika aitwaye Mburia, kwa kulazimishwa mkataba wa mapenzi) "... kwa siku nyingi umekuwa ukinidanganya 
kwamba utanioa mara mjombako atakapokupatia kibali. Sasa chukua hii kalamu na karatasi uandike kwamba utanioa!"
Je, Mureti na Mugiira watajinasua katika mtego wa wasichana hawa ili kutimiza ndoto yao ya masomo huko California? 
Wataweza kurudi Afrika ama watatekwa bakunja na utamaduni mpya wa Wamarekani? Watayaacha masomo watoroke au watafanyaje?
Profesa Ireri Mbaabu ni mhadhiri wa lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Ameandika vitabu kadhaa vya Isimu, 
na maendeleo ya lugha ya Kiswahili.
 

ISBN: 9789966315489 SKU: 2010143001042
KES 485
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect