EAEP Akili Pevu Kiswahili Angaza Grade 5 (Approved)

by S. Otieno, M. Banda


Kiswahili Angaza, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 5 ni kitabu kilichosukwa na kuwambwa kwa makini na kwa kina kirefu. Kitabu hiki kimetosheleza mahitaji ya mtalaa wa umilisi. Kinakuza umilisi uliopendekezwa kwenye mtalaa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo unaomwegemea mwanafunzi zaidi na kumfanya mwalimu awe mwelekezi tu wala si mtoaji wa elimu. Kitabu hiki kitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia kwa stadi za kusikiliza na kuzungumza, Kusoma, Kuandika na Sarufi.
Kitabu hiki kimezingatia: 
• Lugha nyepesi iliyokomaa na inayoweza kueleweka na mwanafunzi kwa urahisi. 
• Mada zilizopangwa kwa kuzingatia mtalaa. Kila mada inaanza kwa picha ambazo zimechorwa vizuri na kikamilifu. Picha hizi zitasisimua hali ya mwanafunzi ya kujifunza. 
• Shughuli mbalimbali ambazo zinawashirikisha wanafunzi wakiwa peke yao, wawiliwawili au katika vikundi. Shughuli hizi zinakuza stadi nyingi za kufikiria kama vile kuchanganua, kutambua, kubainisha na kuhakiki. 
• Ushirikisho wa wazazi na walezi ambao unaimarisha uwajibikaji wa wanafunzi. 
Waandishi wa kitabu hiki wana uzoefu mwingi na wamekiandika kitabu hiki kwa utaalamu mkuu.

ISBN: 9789966564610 SKU: BK00000001869
KES 515
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect