Kurunzi ya Kiswahili Grade 5 Mwanafunzi (Approved)

by A. Matei, J. Mwamburi, F. Wangome, F. Atulo


Kurunzi ya Kiswahili Kitabu cha Mwanafunzi Gredi ya 5 kimeandaliwa kwa ustadi ili kumwezesha mwanafunzi kumudu mtalaa huu unaolenga umilisi kwa njia sahili, yenye mvuto na ya kumjumuisha moja kwa moja kwenye shughuli za ufunzaji.
Kitabu hiki 
• Kimeshughulikia mada kwa njia inayomwezesha mwanafunzi kushiriki kikamilifu katika ujifunzaji. 
• Mada na shughuli za darasani zimeteuliwa kwa uangalifu kumjengea mwanafunzi umilisi wa aina mbalimbali. Mada hizi zinalenga kuimarisha umilisi wa kusikiliza kwa makini, kuzungumza kwa ujasiri, kusoma kwa ufasaha na kuandika vyema. 
• Kuna mazoezi na mijarabu kama vile shughuli kwa mwanafunzi, shughuli ya vikundi, kazimradi, shughuli ya nyumbani na michezo ili kumwezesha mwalimu kupima umilisi wa mwanafunzi kwenye stadi mbalimbali za lugha. 
• Picha halisi na michoro ya kuvutia inamsaidia mwanafunzi katika uelewa wa mada. 
• Kinalenga kumsaidia mwanafunzi kutumia vifaa vya teknolojia kama vile video, redio, tabuleti katika kurahisisha ujifunzaji. 
• Mbinu tofauti za ufunzaji zimejumuishwa kama vile miradi ya uwekezaji, shughuli nje ya darasa, kutumia nyimbo, mashairi, kumhusisha mzazi au mlezi na ujifunzaji katika vikundi. Mbinu hizi zinasaidia kujenga umilisi wa mwanafunzi. 
• Masuala mtambuko na kuhusisha maadili kujenga mada tofauti imeshughulikiwa. 
•Kitabu cha mwalimu kipo ili kumpa mapendekezo katika ufunzaji.

ISBN: 9789966572455 SKU: BK00000001901
KES 603
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect