Kamusi ya Karne ya 21
Kamusi ya Karne ya 21(Toleo la 4) ni kamusi ya Kiswahili yenye uketo zaidi katika karne hii. Imetungwa kwa ustadi wa hali ya juu na wanaleksikografia wenye utaalamu na uzoefu wa uundaji wa kamusi. Ni kamusi inayojivunia upekee unaodhihirisha jinsi lugha ya Kiswahili inavyokwenda na wakati kwa kupanuka katika matumizi yake katika pembe zote za dunia. Toleo hili limeongezwa vidahizovipya zaidi ya 2500 ambavyo vinaashiria maendeleo mapya katika lugha ya Kiswahili. Kamusi hii inaonyesha ukuaji wa Kiswahili na matumizi yake katika nyanja zote za Siasa, Sayansi, Teknolojia ya kidijitali, mitandao ya kijamii, ubadilishanaji wa fedha na bidhaa kupitia kwa mifumo ya kimtandao miongoni mwa mengine.
KES 1,250

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect
UPC | 2010127000480 |
---|---|
Author | Longhorn |
ISBN | 9789987020973 |
Publisher | Longhorn |
SKU | 2010127000480 |