Mentor Kielekezi cha Kiswahili Gredi 5
by E. Andati, K. Chituyi, N. Musyimi na S. Washika
KIELEKEZI CHA MARUDIO YA KISWAHILI GREDI YA 5 KIELEKEZI cha marudio ya Kiswahili Gredi ya 5 kimeandaliwa kwa ustadi ili kumrahisishia mwanafunzi kuelewa mfumo mpya wa elimu ya umilisi. Kitabu hiki:
- Kimeandikwa kumwezesha mwanafunzi kukuza na kujenga ujuzi na uwezo wa kutumia stadi za lugha (Kusikiliza na kuzungumza, Kusoma, kuandika na Sarufi).
- Kimeandikwa kwa lugha rahisi na kutoa mifano mwafaka.
- kimeshughulikia Masuala mtambuko kama vile: uraia, utangamano, elimu ya amani, stadi za maisha, mazingira na teknolojia. - Kina Mazoezi muhimu ili kumsaidia mwanafunzi kufanya marudio.
- Kina Zoezi la Tathmini mwishoni mwa kila sura.
- Kina karatasi sita za Majaribio ya mitihani.
- Kimeandikwa na waandishi wenye tajriba kubwa katika ufundishaji wa somo la Kiswahili katika shule bora nchini Kenya. Aidha, wanaelewa mfumo wa umilisi kwa jumla.