Mazoezi ya Insha Murua kiwango 3

by Story Moja


Kabla ya kuandika insha;

-Fahamu swali au mada ya insha unayoandika. Iwapo huelewi mada na ni insha ya mazoezi mwambie mwalimu mzazi au mlezi akufafanulie.
-Fahamu aina ya insha au hadithi unayotakikana kuandika.
- adika vidokezo vya insha hivyo.

Unapoandika insha;

- Rejelea vidokezo ulivyoandika ili vikuongoze unapoandika insha.
- Tumia maelezo ya uandishi wa insha marua yaliyomo katika kitabu hiki kuandika insha yako.
- Andika insha kwa hati nadhifu ili isomeke kwa urahisi.
- Epuka wasiwasi kuhusu ubora wa insha yako wakati unapoendelea kuandika. Jitahidi tu kadri ya uwezo wako.

Baada ya Kuandika;

- Soma upya insha yako ili uakikishe kwamba inatiririka ipasavyo.
- Soma insha tena ukirekebisha kakosa yoyote yaliomo kama vile ya ngeli, uakifishajitahajia na matumizi ya maneno. Pia rekebisha hatiyako.
- Mpe mwalimu mzazi au mlezi insha yako kisha akupe mawaidha ya jinsi ya jinsi ya kuimarisha uandisha wako.

KES 600
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect