Tata za Asumini

by Said A. Mohamed


"... Zuzu limeerevuka labda, au pengine erevu limezuzuka. Hata yeye Asumini hakuwa na hakika kama alikuwa ZUZU au erevu! Alilokuwa na hakika nalo ni kwamba ndani ya nafsi yake mmeota mawazo yaliyokuwa yakikua mfululizo - nafsi ilizungumza na nafsi mijadala na mabishano, kataa na kubali, lia na nyamaza, hamu na juta, faa na haifai, na ukomo, wakati mwingine ulimfikisha katika kutaka kurudi nyumbani na kisha kughairi tena. Na baadaye kuanza tena upya: kujisaili na kujijibu, kujujadili na kubishana, kukubali na kukataa ... siku zikapita, mpaka ... ... Hivyo ndivyo tunamkuta Asumini, mwanagenzi wa dunia chafu na ngumu: tunamkuta kanaswa katika tata", tokea mwanzo hadi mwisho ... vuta n'kuvute tupu! Ndani, muchuchio wa nafsi yake inayomwita kwa sauti inayotaka ifuate malezi mema ya kuepuka kunajisiwa. Nie, kuna mchuchio mwingine; nguvu tuseme, nguvu zinazomchochea awe mchafu kama walivyo wengine. Huku kakamatwa anavutwa na nguvu za ndani, na huku kakamatwa anavutwa na nguvu za nje; kasi, kasi, kasi ... hadi anararukararuka! Mwandishi wa riwaya hii ameandika vitabu vingi vya riwaya, tamthilia, ushairi na tahakiki ya fasihi. Baadhi ya kazi zake mashuhuri ni Asali Chungu, Utengano, Dunia Mti Mkavu, Sikate Tamaa, Kina cha Maisha, Pungwa, Mwongozo wa Kilio cha Haki... Karibuni hivi, mwezi wa Disemba, 1988, alitunukiwa zawadi ya Uandishi bora kabisa (kitaifa) wa riwaya huko Tanzania - zawadi iliyotolewa na Chama cha Waandishi, Tanzania.

SKU: 2010143000072
KES 499
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 3,000
Free click & collect