Vipawa Vya Hasina 8e

by Said A Mohamed


Vipawa vya Hasina 8e ni kitabu kinacholenga wanafunzi wa Darasa la Nane katika shule za msingi ili kuendeleza na kukuza uwezo wao wa kusoma.<br />Miongoni mwa sifa za kipekee za kitabu hiki ni:

  • masimulizi rahisi kwa njia ya hadithi, usimulizi kwa nafsi ya kwanza umoja, mbinu rejeshi na uzungumzi nafsia.
  • kuingiza ucheshi katika maandishi kupitia masimulizi, dayolojia, misemo, methali, taharuki, tashibihi, tashihisi, takriri, kejeli, chuku, taswira, tanakali za sauti na picha za rangi zenye kusisimua.
  • kuwapitisha na kuwalea wanafunzi katika mazingira ya maisna ya nyumbani, shuleni, kijijini na jijini, malezi, mila ya ndoa za wasichana wadogo, afya, ujana na matatizo yake, umuhimu wa teknolojia, habari na mawasiliano, michezo, uwajibikaji, stadi za maisha, kazi, utu, uvumilivu, uadilifu, jinsia, haki za binadamu, haki za watoto, kuishi kwa utangamano na amani.

Mradi wa Kusoma ni mfululizo wa vitabu vya ziada ambao unaambatana na kozi ya Kiswahili Sanifu.

ISBN: 9780195734560 SKU: 2010143000411
KES 360
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect