Kamusi Rasmi ya Picha

by Yahya Mutuku


Kamusi rasmi ya picha imeandikwa kwa upekee usiodhihirika katika kamusi nyingine. Kamusi hii ina sifa zifuatazo:

  • Imeepuka mpangilio wa kialfabeti uliotumiwa na kamusi nyingine. Msamiati umepangwa kwa makundi badala ya kialfabeti kwa sababu wanafunzi katika kiwango hiki bado hawawezi kusaka msamiati kialfabeti (kiabjadi).
  • Mkusanyiko wa msamiati unaambatana na ule ulio katika silabasi ya Kiswahili iliyoidhinishwa na taasisi ya elimu nchini (awali Kenya Institute of Education, sasa Kenya Institute of Curriculum Development).
  • Kamusi hii ina picha maridadi zinazomvutia mwanafunzi na kumrahisishia kazi.
  • Picha zote zimeambatanishwa na maelezo kabambe na kwa lugha nyepesi inayomfaa si mwanafunzi pekee bali mtu yeyote akipendaye Kiswahili.
  • Msamiati uliotumika utamwezesha mwanafunzi kujua mengi kwenye mazingira yake.
ISBN: 9789966478351 SKU: 2010127000526
KES 696
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect