KLB Visionary Kiswahili Mwanafunzi Grade 5 (Approved)


KLB Visionary Kiswahili Gredi ya Tano (Kitabu cha Mwanafunzi) kimechapishwa kwa kusudi la kuendelea kuimarisha uwezo wa mwanafunzi katika lugha ya Kiswahili kupitia Sarufi na stadi za lugha; Kusikiliza, kuzungumza, Kusoma na kuandika.
• Kitabu hiki kimechapishwa kwa kuzingatia mtaala mpya wa kiumilisi kutoka Taasisi ya Ukuzaji Mitaala
Nchini Kenya (KICD) wa mwaka wa 2019 wa masomo ya shule za msingi, gredi ya tano. 
• Mwanafunzi amepewa nafasi ya kutosha ya kutambua na kujifunza mambo mapya ili kukuza uwezo
wake wa kukabili mambo katika maisha. 
• Mazoezi ainati, mifano na picha zimetumika kwa nia ya kulenga mazingira ya mwanafunzi na usasa ili
kumrahisishia ujifunzaji. 
• Masuala mtambuko na ya kijinsia yamejumuishwa kitabuni ili kukuza mwanafunzi anayewajibikia mabadiliko maishani. 
• Kitabu hiki kimekuza upekee wa kutumia shajara na kazi mradi katika sehemu ya mwisho ya kila mada. Shajara na kazi mradi zimekusudiwa kumsaidia mwanafunzi kutumia ujuzi wa mambo aliyogundua au kujifunza kutokana na mada husika ili kubuni kitu kipya au kutatua suala fulani katika maisha ya kila siku.

KES 418
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 3,000
Free click & collect