Msingi wa Fasihi Simulizi


Msingi wa Fasihi Simulizi ni Kitabu kinachozitalii kwa upana dhana za kimsingi katika utanzu wa fasihi simulizi. Kitabu hiki kinawapa wanafunzi na walimu wa fasihi simulizi kwa Kiswahili msingi jadidi katika taaluma hii. Vipera mbalimbali vya fasihi simulizi vimefafanuliwa kwa undani huku mifano maridhawa ikitolewa kutoka jamii anuwai barani Afrika na kwingineko. Istilahi kadhaa zinazotumiwa katika uchambuzi wa fashihi simulizi zimejadiliwa kwa namna ya kipekee. Maswali ya kudurusu yametolewa ili kumhami vilivyo mwanafunzi wa fasihi simulizi. Kitabu hiki kitawafaidi wanafunzi, walimu, wasomi na wapenzi wa fasihi simulizi kuanzia shule za upili hadi vyuo vikuu. Waandishi; Prof. Kitula King'ei na Bi. Catherine Kisovi ni walimu na wataalamu wenye tajriba pana katika uandishi na ufundishaji wa Kiswahili katika viwango mbalimbali.
KES 564
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect
Author Kingei
ISBN 9966446001
SKU2010143000111

Reviews

Leave a product review
or cancel