Safari ya Lamu

by John Habwe


Safari inayoanza Nairobi inampa Musa nafasi ya kutafakari, kujionea fahari, kuiona bahari na zaidi, kujiathiri. Anapofika Lamu, Musa anapatana na Maimuna; msichana mrembo mwenye hulka na falsafa ambaye kwa usuhuba wake anamwonjesha Musa tamu na chungu. Anampitisha Musa barabarani na vichochoroni kisiwani Lamu. Hatimaye, Musa anafahamikiwa kuwa, “...Lamu ilicheka usiku. Lamu iliterema usiku. Lamu ilitembea usiku. Mchana ililala. Wanawake hawaoni mchana.

Kumbe wakati wote huu Musa amekuwa akistarehe na mke wa mtu. Tena mtu mwenyewe ni mganga! Najina lake...Mkuki! Na mkuki kazi yake ni kuchoma. Safari ya Lamu si tamu tena! Kwa nini Musa akasafiri hadi Lamu kustarehe na mke wa mtu ilhali nyumbani mkewe; Maria, anamngoja ili amwandalie starehe zote? Sasa amechomwa na Mkuki. Nani amfanyie dawa? Mamakeaumkewe?

ISBN: 9789966499042 SKU: 2010129000106
KES 664
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect

Reviews

This product does not have any reviews yet.

Add your review