Daraja la Mafanikio (One Planet)

by Assumpta K.Matei


... alipoyatazama macho ya mama yake, aliona kwamba yalikuwa yametwaa wekundu. Hakuwa na haja ya kuuliza kiini cha jambo hilo. Hakuwa na wakati wa kurudia yaliyopita. Alijiona kama mto ambao ukipitia mahali hauparudi...

Moja kati ya mambo ambayo jamii imelenga shabaha kuyafikia ni kumjengea mwanafunzi mazingira ambayo yatampa fursa ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji bila kubaguliwa kwa misingi yoyote.

Je, wanajamii wako tayari kutekeleza hili? Wako radhi kuhakikisha kwamba wameangamiza kabisa vizingiti ambavyo vinawazuia vijana kujiunga na shule na kuhitimu? Wako radhi kumpa mwanafunzi uwanja mpana wa kujifunza kwa kuyatalii mazingira na hapo hapo anaitumikia jamii yake?

Abiri chombo cha Mikaili, Ezra na Bi. Shali katika, Daraja la Mafanikio. Jipakulie maadili shibe yako kutokana na tajiriba:zilizomo.

ISBN: 9789914410099 SKU: BK00000011681
KES 320
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect