
Kiboko alivyochukia Chura
by H.Rajab
Paukwa Pakawa ni mfululizo wa visa, mikasa na ngano zilizotungwa ili kuwapa watoto wanaochipuka katika mafunzo, chanzo chema. Lugha imerahisishwa na matukio yamepewa msisimko utakaowafurahisha watoto wote wa nasari, pri-uniti hadi darasa la pili, huku wakijimudu katika kuifahamu lugha ya Kiswahili. Kiboko Alivyomchukia Chura ni hadithi ya marafiki wawili wanaokumbwa na njaa kwa sababu ya ukame na umaskini. Wanaamua kujitafutia kazi kwa tajiri mmoja mwanadamu. Wanapoajiriwa, wanashikwa na tamaa ambayo inatisha urafiki wao. Je, mambo yanakuwa vipi?
KES 202

International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect