Kovu Moyoni


"Hapa duniani si Makao yetu. Makao yetu yako mbinguni... Juu hakuna maradhi wala hakuna kifo. Hakuna hata nondo wa kuiba chochote ghalani." Kovu Moyoni ni hadithi ya kusisimua inayosimulia matukio katika kijiji cha Siloko katika nchi huru ya Tandika. Inahusu mapambano ya mjane mmoja dhidi ya utawala dhalimu unaolinda na kulifadhili genge la Wanamgambo la vijana wanaoshambulia na kupora kijiji cha Siloko kwa kisingizio cha kuondoa watu wasio wenyeji. Serikali ambayo Boke anatarajia imlinde na mali yake inafeli katika jukumu lake la kimsingi na badala yake inalinda kundi lenye uwezo mkubwa la wanyakuzi wa ardhi na mibabe wa kivita.

KES 605
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect
Author John Habwe
ISBN 978996655354
SKU2010143000758

Reviews

Leave a product review
or cancel